Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima mpunga walamba ruzuku mil. 478/-

MPUNGA Wakulima mpunga walamba ruzuku mil. 478/-

Sat, 3 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mkataba huo wa miaka minne ulitiwa saini uzi kati ya Mratibu wa Shughuli za USADF, Gilliard Nkini na viongozi wa kampuni ya wakulima wa mpunga wa kijiji hicho.

Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba huo, Nkini alisema lengo la kutoa ruzuku hiyo ni kuongeza ubora wa mazao yanayozalishwa na wakulima wa kijiji hicho ili kuinua uchumi wao na kuwa na uhakika wa chakula.

Nkini alisema si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kuwasaidia wakulima kwa kuwa awali ilitoa ruzuku ya Sh. milioni 200 mwaka 2016 na baada ya kuona  wamefanya vizuri, iliamua kuongeza kiwango.

“Fedha hizi ni kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao. Mkuu wa USADF, Elizabeth Feleki, ameridhishwa na kazi yenu ndiyo maana ameamua kuwaongezea ruzuku na hii ruzuku itatolewa mpaka mwaka 2024,” alisema.

Viongozi wa Kampuni ya Wakulima ya Azimio Mswiswi High Quality Rice Millers yenye zaidi ya wakulima 300, walisema mbali na wanachama wao kunufaika na ruzuku hiyo pia na vijiji vingine saba vya jirani vitanufaika.

Katibu wa Kampuni hiyo, Luquman Shirima, alisema watazitumia fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia mazao pamoja na kununua mashine ya kisasa ya kukoboa mpunga.

Alisema watazitumia pia kuongeza mtaji wa wakulima ili kuhakikisha wanaongeza uzalishaji na kufikia hatua ya kujitegemea endapo wafadhili wataacha kuwapelekea fedha za kuendeleza shughuli za kampuni yao.

 “Tunashukuru kampuni hii kwa ruzuku hii. Wakulima tutaongeza uzalishaji na kuongeza ubora wa mazao yetu. Kwa  sasa tutaongeza nguvu ya kutafuta soko la mazao yetu ili wakulima wanufaike zaidi,” alisema Shirima.

Baadhi ya wakulima wa mpunga, waliiomba serikali iwasaidie kuboresha miundombinu ya barabara ili wawe wanasafirisha vizuri mazao yao kutoka shambani kwenda kwenye maghala pamoja na kusafirisha pembejeo kwenda mashambani.

Mmoja wa wakulima hao, Andrea Mwambenengo, alisema kutokana na ubovu wa barabara za eneo hilo baadhi ya magari makubwa yamekuwa yakishindwa kuingia na kutoka wakati wa kusafirisha mazao, hivyo kulazimika kutumia matrekta.

Alisema watashirikiana na viongozi wao kuendelea kuiomba serikali iwaboreshee miundombinu hiyo ili wasafirishe mazao yao kwa urahisi zaidi.

Mbarali ni miongoni mwa wilaya za Mbeya ambazo uchumi wa wananchi wake unategemea zaidi kilimo cha mpunga.

Chanzo: ippmedia.com