Wakulima 949,643 wamenufaika na mbolea ya ruzuku hadi kufikia Juni mwaka huu kati ya milioni 3.3 waliosaijiwa tangu utaratibu uanze Agosti mwaka jana.
Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 17,2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dk Stephen Ngailo wakati taarifa ya utekelezaji na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2023/24.
Hata hivyo, amesema lengo la kuwasajili halikuwa ni kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku bali na kupata huduma nyingine ikiwemo za ugani na pembejeo.
“Kiasi cha mbolea ya ruzuku kilichonunuliwa kwa ruzuku ni tani milioni 3.36 hadi kufikia Juni mwaka huu,” amesema.
Kwa mujibu wa takwimu za mamlaka hiyo mkoa wa Mtwara unaongoza kwa ununuzi wa mbolea hiyo baada ya kununua tani 332,602, Ruvuma (323,947) na Simiyu (220,094).
Pia kwa upande wa mikoa iliyonua kidogo na tani walizonunua katika mabano kuwa ni Dar es Salaam (5431), Mara (40,267) na Shinyanga (58,003).