Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima kunufaika na zana za kisasa

B38346F6 976C 4699 A808 1B87ADBFEC06.jpeg Wakulima kunufaika na zana za kisasa

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema ili kukuza uzalishaji katika kilimo, wananchi wanahitaji kuwa na na zana bora za kilimo.

Akizungumza leo Agosti 6 wakati wa utiaji saini wa makubaliano (MoU) kati ya benki ya Stanbic Tanzania (SBT) na kampuni ya zana za kilimo ya AgriCom Africa (AA) kwa ajili ya upatikanaji wa zana bora za kilimo katika viwanja vya Nane Mkoani Mbeya, Homera amesema Nyanda za juu Kusini inaongoza kwa kilimo nchini, hivyo makubaliano haya yatasaidia wakulima kuondokana na zana duni badala yake watatumia mashine za kisasa katika uzalishaji.

"Kilimo cha sasa ili ufanikiwe unahitaji mashine za kisasa hivyo makubaliano haya ya kuwawezesha zana za kilimo wakulima kati ya benki ya Stanibic ambao wako karibu afrika nzima wataweza kurahisisha kilimo hatimae kusaidia adhima ya serikali kwamba ifikapo mwaka 2030 Tanzania iongezeke kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa asilimia kumi,"

Awali akizungmza katika hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mikopo ya Asseti na Vyombo vya Moto kutoka SBT (Head of Vehicle Asset Financing), John Mosha amesema kuwa kupitia ushirikiano huo, wananchi husussani wakulima kuwawezesha kununua zana za kilimo sambamba na kukopa vifaa na mashine ili kuongeza ufanisi na uzalishaji wenye tija.

“Ushirikiano huu utakakikisha upatikanaji wa zana za kisasa ambazo ni bora. Wakulima watanufaika na zana hizi za kisasa zitakazoweza kusaidia kuongeza uzalishaji kwenye shughuli za shamba, hivyo kuhamasisha maendeleo ya kilimo biashara kwa kuleta mapinduzi ya kiuendeshaji hali itakayochangia kukuza mafanikio ya sekta ya kilimo biashara nchini.” amesema Mosha.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka SBT, Fredrick Max amesema benki hiyo imeamua kuja na mpango huu uliojikita katika kukuza mnyororo wa thamani kwenye kilimo biashara kwa kubuni mifumo inayoweza kuongeza uzalishaji, uchakataji na usafirishaji wa mahitaji katika kilimo.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za AgriCom (AgriCom Group), Alex Duffar makubaliano hayo yanalenga kuchagiza matumizi ya zana za kilimo ambazo ni bora na za kisasa kwenye kilimo, hivyo kukuza uchumi na maendeleo ya viwanda nchini.

“AgriCom Africa tumejizatiti kuhamasisha matumizi ya zana za kilimo kupitia ushirikiano kama huu ambao leo tumeuingia na Stanbic Bank Tanzania.

“Ushirikiano huu utasaidia wakulima kukopa fedha za kununulia zana bora za kilimo. AgriCom Africa ikiwa ni kampuni inayojulikana kwa ubunifu wake katika zana za kilimo,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live