Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima kahawa wapewa siri ya ongezeko la mavuno

7125 20150818 Coffee Beans Shutterstock 71813833 Wakulima kahawa wapewa siri ya ongezeko la mavuno

Tue, 14 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKULIMA wa kahawa mkoani Kagera wametakiwa kuonyesha ushirikiano kwa wataalamu wa kilimo wanapofika shambani kutoa elimu ya ufufuaji mashamba na upandaji miche bora, ili kuleta tija kwa zao hilo.

Imeelezwa kuwa ushirikiano huo kati ya mkulima na mtaalamu utasaidia ongezeko la mavuno kwani kumekuwapo changamoto za uzalishaji unaosababisha mavuno kidogo ya kahawa tofauti na matarajio ya mkulima.

Hayo yalielezwa na baadhi ya wataalamu wa kilimo katika wilaya za mkoa huo, ambao walipatiwa mafunzo ya ujuzi wa kushawishi mkulima kujifunza kupitia mashamba darasa.

Elizabeth Ndaba kutoka wilayani Kyerwa, alisema kwa kiwango kikubwa wakulima wamekuwa wakitegemea kilimo cha kahawa kama sehemu ya kupata uchumi.

Alisema tatizo linalowakumba ni kutokuwa na elimu ya ufahamu wa kutunza shina la mbuni wa kahawa, ambao unategemewa kwa uvunaji na kwamba kupitia wataalamu, wataonyesha mabadiliko kwa kukubali kushiriki katika elimu ya vitendo.

“Kinachoangaliwa hapa kwenye mafunzo ni kusaidia mkulima kwa kuonyesha vitendo vya ushiriki namna ya kuandaa na kupanda hadi kutunza mche wenye tija, unatarajiwa kuwa na mavuno mengi,” alisema Ndama.

Silaji Ismail kutoka Wilaya ya Missenyi, alisema ili kuleta mabadiliko yanayotazamiwa kwa mkulima na kufufua zao la kahawa, vijana mijini na vijiji wajitoe kwa kuelimisha wakulima.

Alisema mwaka 2016 mibuni ilipata ugonjwa wa manjano (mnyauko) ulisababisha baadhi ya wakulima kuendelea na kilimo hicho, ingawa waliendelea kuwa tegemezi kutokana na kushindwa kujipatia kipato kwa ajili ya familia.

Meneja Mradi wa Café Africa mkoani Kagera, Daniel Mwakalinga, alisema uzingatiaji wa elimu ya mashamba darasa yatakayotumika kufundishia mkulima ili kujua namna ya uchipulishaji wa mashamba yao tija kwa mkulima itaongezeka.

Aliongeza kuwa wataalamu ngazi ya kata, wilaya na wakulima kupitia vyama vikuu vya ushirika Kagera Coperative Union 1990LTD (KCU) na Karagwe Distric Cooperative Union (KDCU) watashiriki kusaidia mkulima kuongeza uzalishaji wa tija.

Alisema kipindi hiki cha wakulima wanatakiwa kwenye mavuno na kwamba mradi umeanda wataalamu 40 wenye uwezo wa kutoa elimu ya kutatua changamoto ya mashamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live