Wakulima wa mazao ya mafuta haswa alizeti wametakiwa kuongeza uzalishaji wa mazao hayo ili kukidhi mahitaji ya viwanda vya uzalishaji wa mafuta nchini, kwani viwanda vingi vya bidhaa ya mafuta vinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa malighafi.
Hayo yamesemwa na waziri wa viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji alipofanya ziara katika kiwanda cha mafuta cha Wilmar Tanzania Limited, ambapo amesema Tanzania inazalisha asilimia 40 pekee ya mafuta yanayohitajika nchini, huku mwakilishi wa kiwanda hicho akisema wanaendelea kushirikiana na serikali haswa katika kusaidia wakulima wadogo wa mazao hayo.
Pia Dk. Kijaji ametembelea kiwanda cha sabuni kinachomilikiwa na Wilmar ambacho kimezalisha ajira Zaidi ya 100 Kwa vijana wa Tanzania, baada ya hapo akatembekea kwenye kiwanda cha utengenezaji wa kamba na ngazi cha Dar es Salaam Rope