Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima Tunduru wagoma kuuza ufuta

Ufuraaaaaaaaaaaaaaaaaa Ed.webp Wakulima Tunduru wagoma kuuza ufuta

Sat, 20 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKULIMA wa ufuta wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, wamegoma kuuza zao hilo kutokana na bei ndogo iliyotolewa na wanunuzi.

Kutokana na hali hiyo wakulima hao wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuingilia kati kwa kuwatafutia wanunuzi watakao toa bei nzuri.

Hayo yalijitokeza wakati wa mnada wa sita uliofanyika viwanja vya ofisi za Chama cha Ushirika cha Mlingoti Magharibi Amcos kwa kujitokeza wanunuzi wawili kwa bei ya Sh. 1,750.

Mwingine aliomba kununua kwa Sh. 1,730 ikiwa ni kabla ya makato ya kisheria.

Mbina Mnanka, Mohammed Salumu na Bakari Selemani wakizungumza na waandishi wa habari, walisema kwa mtazamo wa kawaida inaonyesha kuwa wanunuzi wanaojitokeza ni madalali ambao wamelenga kujinufaisha kupitia migongo ya wakulima.

Walisema wana imani na serikali katika utendaji wake na kwamba haiingi akilini katika mnada uliopita ufuta wao uuzwe kwa bei ya wastani wa Sh. 2,047.26 wiki moja baadaye bei ishuke kwa wastani wa Sh. 400.

Walisema bei hizo siyo rafiki kwa mkulima na hazizingatii gharama alizotumia wakati wa kuandaa shamba, kulima, kupalilia, kupulizia dawa na kuvuna.

“Bei zinazotolewa na madalali wa wanunuzi hao kwa kisingizio cha kushuka kwa bei za soko la dunia kutokana na corona, zinatukatisha tamaa wakulima kuendelea kulima zao hilo ikilinganishwa na gharama tunazotumia kuhudumia mazao yetu,” alisisitiza Mnanka.

Wakulima hao pia walionyesha shaka kuwa huenda madalali hao wanafanya hivyo kutokana na kutokuwapo kwa ushindani wa kampuni zingine katika minada hiyo ambayo tangu ianze wanunuzi ni walewale.

Awali, mwakilishi wa Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakuliwa wilayani Tunduru (TAMCU), Imani Kalembo, Yasini Masiano, aliwataka wakulima walioshiriki mnada huo kuwa makini kusikiliza bei zinazosomwa kwenye barua za wanunuzi ili waweze kuchagua bei kubwa kuliko zote.

Akiahirisha mnada huo, Makamu Mwenyekiti wa TAMCU, Mussa Manjaule, alisema chama hicho kimeungana na uamuzi wa wakulima hao na kueleza kuwa mnada wa marudio utafanyika Juni 20, mwaka huu.

Alisema ingawa bei zinaendelea kushuka ikilinganishwa na bei za awali, iliyotolewa na wanunuzi hao siyo rafiki na haiwashawishi wakulima kuendeleza zao hilo kwa msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live