Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima Kilimanjaro wapewa somo Mabadiliko Tabianchi

Kilimo Kilimanjaro Wakulima Kilimanjaro wapewa somo Mabadiliko Tabianchi

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wanaolima kilimo cha umwagiliaji mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufuata maelekezo ya wataalamu na kuhakikisha wanayatumia vizuri maji yaliyopo ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Rai hiyo imetolewa Januari 20, 2022 na Meneja wa Tume ya umwagiliaji Mkoa wa Kilimanjaro, Said Ibrahimu wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi kuhusu hali ya maji kwa sasa, ambapo pia amewataka wakulima kuweka kipaumbele katika kulima mazao yenye tija ambayo yanazalisha vizuri.

Ibrahim amesema tume hiyo tayari imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha hali ya ukame, ikiwemo kuelimisha wakulima kulima kilimo cha matone pamoja kuangalia maeneo yanayofaa kujenga mabwawa.

Amesema wakulima wasipozingatia elimu inayotolewa na maelekezo ya wataalamu wakaendelea kulima kiholela siku zijazo kunaweza kuwa na athari kubwa zaidi katika kilimo.

"Kutokana na mabadiliko haya ya tabianchi, sisi kama taasisi tumechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuelimisha wananchi kuhusiana na kilimo cha matone, lakini pia kujenga mabwawa, ambayo yatatumika kuzuia mafiriko ambayo yanatokana na maji yanayoanzia kwenye miinuko mikubwa na kuhifadhi maji ambayo yatatumika kwenye kilimo cha umwagiliaji," amesema Ibrahim.

"Wakulima wazingatie utaalamu unashauri nini, lakini pia walinde mifereji na kuwa sehemu ya uboreshaji wa mifereji ambayo imekuwa na changamoto ya utoroshaji maji na siyo kila kitu wasubirie serikali ifanye," amesema.

Advertisement Ameongeza kuwa, "Pia tumeendelea kuimarisha na kuboresha miundombinu ya maji ikiwemo mifereji ambayo imekuwa ikipoteza maji kwa kiasi kikubwa na tumeendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi wazingatie kanuni bora za maji kwa sababu hitaji la maji ni kubwa na hali hii haikutarajiwa kabla."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live