Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima Chato kunufaika na Ziwa Victoria

Lakevictoria Wakulima Chato kunufaika na Ziwa Victoria

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia bajeti ya mwaka 2023/2024 imepanga kuboresha mifumo ya umwagiliaji kwa wakulima wa Chato walio pembezoni mwa Ziwa Victoria kwa kuweka Pampu kubwa za kuwezesha kilimo cha umwagiliaji kwa kuvuta maji kutoka ziwani kwenda katika mashamba.

Hayo yamesemwa Jana Jumanne Julai 11, 2023 na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde katika wilayani Chato aliposhiriki zoezi la uzinduzi wa kampeni ya mapinduzi ya kilimo na uchumi wilayani hapo.

"Rais Samia amekipa kilimo kipaumbele na kuwajali wakulima wa nchi hii, hilo linajidhihirisha kwa ongezeko la bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka Sh294 bilioni miaka miwili iliyopita hadi kufikia Sh970 bilioni mwaka 2023/2024,”amesema.

Awali, Mbunge wa Chato Mheshimiwa, Dk Medard Kalemani alishukuru Serikali kwa jinsi inavyoendelea kuikumbuka Chato katika sekta ya kilimo ikiwemo mpango wa ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji ya Nyisanzi na Mwabasabi, ukarabati na ujenzi wa skimu mpya za umwagiliaji ili wakulima wazalishe kwa tija.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live