Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima 83,000 kupewa mbolea ya bil 16.5/-

388505148e5cdc008b1fbfa0ddcf61ba Wakulima 83,000 kupewa mbolea ya bil 16.5/-

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Tabora Dk Philemon Sengati amezindua usambazaji mbolea bure unaojulikana kama 'Action Africa'.

Zaidi ya tani 12,500 za mbolea aina ya YaraMila Cereal yenye thamani ya shilingi bilioni 16.5 itasambazwa kwa wakulima nchini.

Uzinduzi huo umefanyika jana wilayani Nzega, jumla ya wakulima wadogo 83,000 nchini Tanzania watanufaika kwa kupata mbolea hiyo bila malipo.

Dk Sengati alisema, Serikali imeamua kukifanya kilimo kuwa cha kibiashara na kuwaletea maendeleo na wafurahie shughuli ya kilimo.

Alitoa wito kwa wakulima wadogo wanajisajili ili waweze kupata mbolea kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mahindi na mpunga.

Alisema wakulima ambao watanufaika ma mradi huo wataweza kuongeza uzalishaji wa mahindi katika ekari moja kutoka maguni 2 na kupata magunia 25.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yara Tanzania Winston Odhiambo alisemachini ya mpango huo, mkulima atahitajika kujisajili kupitia namba *149*46*16# na kwamba, kitambulisho cha mpigakura na cha taifa vitatumika kukamilisha usajili.

Odhiambo alisema lengo la mradi huo ni kukuza uzalishaji wa mahindi na mpunga ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na chakula kingi na hivyo kuwa na usalama wa chakula.

Alisema chini ya mpango huo watagawa mifuko mitatu kwa ajili ya ekari moja ya mahindi na mifuko miwili kwa ajili ya ekari ya mpunga.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisema Serikali haitasita kumkamata na kumshitaki kama muhujumu uchumi msambazaji au mtu atakayekutwa akiuza mbolea hiyo kwa kuwa inastahili kutolewa bure kwa wakulima wadogo.

Alisema lengo mpango pamoja na kuongeza usalama wa chakula nchini ni kuwainua wakulima wadogo ili wakuze kilimo chao kwa nia ya kuwa na uwezo ya kujinunulia mbolea wenyewe.

Bashe aliongeza kuwa chini ya mpango huo wakulima pia watapata punguzo la mbegu za mahindi ambapo watanunua kwa shilingi 5500/= badala ya shilingi 12,500/- kwa mfuko wa kilo mbili.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Advera Bulimba alisema zaidi ya wakulima wadogo 4,000 wamejisajili na wanakusudia kufikisha wakulima 10,000 wilayani humo.

Chanzo: habarileo.co.tz