Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima 32, 000 kufundwa kuzuia upotevu wa chakula

Auawa Baada Ya Kuiba Mahindi Wakulima 32, 000 kufundwa kuzuia upotevu wa chakula

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Zaidi ya wakulima 32, 000 wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameelimishwa jinsi ya kuepuka upotevu wa mazao wakati wakuvuna shambani na kusafirisha.

Akizungumza na wakulima wa Kata ya Ngofila na Lagana wilayani humo jana Aprili 16, 2023, Msimamizi wa Kitengo cha Kilimo na Uchumi kutoka Shirika la World Vison Tanzania Kanda ya Ziwa, Samwel Maganga amesema baada ya elimu hiyo wataondokana na changamoto ya kupoteza mazao kwa asilimia 40.

Amesema baada ya kubaini changamoto ya upotevu wa mazao na kusababisha upungufu wa chakula kwenye kaya kutokana na wakulima kutokuwa na uelewa, wameanza kutoa elimu kupitia mradi wa Nurish unaolenga kuwawezesha wananchi kuwa na lishe bora, uhakika wa chakula pamoja na kupunguza umasikini kwenye ngazi ya kaya kwa kufanya shughuli zingine za maendeleo.

“Wakulima wengi hawana uelewa wa kuvuna mazao yao vizuri ili yasipotee,tuna shirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa hakuna upungufu wa chakula ambapo awali upotevu ulikuwa unasababisha upungufu wa chakula kwenye kaya 3500,”amesema

Baadhi ya wakulima akiwemo Masanja Njile na Juma Paul wakazi wa Kijiji cha Ngofila wamekiri kuwepo changamoto ya upotevu wa mazao kutokana na kutojua njia bora inayowawezesha kuzuia upotevu huo ili wawe na chakula cha kutosha huku wakiiomba Serikali kufikisha elimu hiyo kwa wakulima wengi.

Ofisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ansila Karani amewataka wakulima kuendelea kulima mazao yanayostahimili ukame ukiwemo uwele na mtama kutokana na Wilaya hiyo kukabiliwa na ukame na mazao mengine kushindwa kuhimili.

Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jaquiline Kaihura amesema mradi wa Nurish utachangia kuleta mabadiliko katika suala la lishe ili kuiwezesha jamii kuwa na afya bora na kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Chanzo: mwanachidigital