Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulia malighafi za kutengeneza bia kupigwa jeki

POMBE Wakulia malighafi za kutengeneza bia kupigwa jeki

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Ripoti ya 'Tanzania in Figures 2022' inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikionyesha uzalishaji bia nchini ukiongezeka mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka 2021, wadau wa sekta hiyo wamekuja na mbinu kuhakikisha bidhaa hiyo ya starehe inazidi kuongezeka.

Takwimu hizo zinaonyesha mwaka 2021 uzalishaji wa bia ulikuwa ni lita milioni 380 kisha kuongezeka hadi kufikia lita milioni 456 mwaka 2022, licha ya kuwapo kwa panda shuka inayodaiwa kuchangiwa na upatikanaji wa malighafi.

Akizungumza katika Maonyesho ya Nanenane mkoani Dodoma Agosti 8, 2024 Ofisa Kilimo wa Kampuni ya uzalishaji bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL), Jacob Mwavika amesema ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo wanawawezesha wakulima wa malighafi zinazotengeneza bia ili kuongeza tija.

“Kwa muda mrefu, tumekuwa tukichukua hatua mbalimbali za kuwasaidia wakulima wadogo hapa nchini ikiwamo kutoa mafunzo ya kitaalamu, vifaa vya kilimo na pembejeo muhimu kwa wakulima.

"Pia, tumefanikiwa kuingia mikataba na wakulima wengi ambao mazao yao yanatumika katika utengenezaji wa bia katika kiwanda chetu ili tuongeze tija na uzalishaji," amesema na kuongeza Mwavika.

Malighafi zinazohusika katika utengenezaji wa bia na vileo vingine ni pamoja na mazao ya: Shayiri, mtama na zabibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live