Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajasiriamali wafunzwa kufuga kuku

74139e4a65a82942ddc12b39e8d96f0b Wajasiriamali wafunzwa kufuga kuku

Mon, 31 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAJASIRIAMALI wa Jiji la Arusha wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi kwa kuwawezesha kupata mafunzo yakiwemo ya ufugaji kuku, utengezaji batiki na kuunganishwa na fursa za mikopo katika benki za NMB na CRDB.

Wamesema ni nadra kwa kiongozi kama huyo, kutoa elimu bure kwa wajasiriamali kuhusu utotoleshaji vifaranga, utengezaji batiki, utengezaji sabuni za unga na maji, kupanda vitunguu na kutengeneza pilipili.

Walisema elimu waliyopata wataitumia vema kujikwamua kiuchumi na kupata mikopo katika benki hizo, kwa kuwa bidhaa watakazozalisha zitakubalika .

"Tunashukuru DC Kihongosi kwa sababu si mchoyo wa fursa za kimaendeleo, tumejifunza jinsi ya kutotolesha vifaranga wengi kwa njia za boksi la kawaida, utengezaji wa sabuni na mengi "alisema mjasirimali Lilian Joseph.

Mjasiriamali mwingine, Issa Mohamed alisema utengezaji batiki ni mojawapo ya fursa zilizopo sokoni. Alisema kwamba watatengeneza vikoi vya aina mbalimbali kwa sababu Jiji la Arusha ni la utalii, hivyo kuwezeshwa kwa mafunzo hayo kutawawezesha kutoka kwenye umasikini.

Kihongosi alisema ameamua kutoa mafunzo hayo kwa siku mbili, kuwezesha wajasiriamali kujikwamua kiuchumi. Alisema amepigwa vita na watu, wakidai kazi ya ukuu wa wilaya ni kuwatumia wananchi na si kutoa mafunzo kwa wajasiriamali.

Alisema ameamua kutoa elimu hiyo kwa wajasiriamali wajikwamue kiuchumi, kwa kwa yeye awali alipomaliza chuo hakupata ajira serikalini, bali aliajiri katika ujasiriamali ukiwemo kufuga nyuki.

"Nimeamua kutumia elimu yangu kuwasaidia wajasiriamali hawa sambamba na kuwaunganisha na masoko ikiwemo fursa za kibiashara kwa kukopa benki hizo mbili ili wajikwamue kiuchumi"alisema Kihongosi.

Chanzo: habarileo.co.tz