Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajasiriamali Tanzania watakiwa kujipanga kueleka uchumi wa kati

Wajasiriamali Tanzania watakiwa kujipanga kueleka uchumi wa kati

Sat, 21 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kituo cha ujasiriamali cha CEED Tanzania kimewataka wajasiramali nchini kujipanga wakati Tanzania ikielekea katika uchumi wa kati.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na CEED Tanzania inaeleza kuwa kituo hicho kiliandaa mafunzo ya wajasiriamali mkoani Morogoro kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kukuza biashara zao.

Akizungumza katika mafunzo hayo, mkurugenzi wa kituo hicho, Atiba Amalile amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha kusimamia biashara, kutatua changamoto na kutafuta fursa za biashara.

“Haitakuwa biashara kama kawaida wakati Tanzania itakapokuwa nchi ya kipato cha kati miaka ijayo,”  alisema Amalile.

Mshauri wa masuala ya kodi na mwakilishi wa CEED Tanzania jijini Dodoma, Baptist Mnyapale  aliwahimiza wajasiriamali wa Morogoro kufahamu kanuni zinazoathiri biashara zao moja kwa moja.

Aliwataka kuwa na ufahamu wa masuala ya kodi ikiwa ni  pamoja na kanuni na sheria zinazoweza kuathiri biashara zao.

“Mhakikishe mnafahamu kanuni na sheria zinazoweza kuingilia na kuathiri biashara zenu moja kwa moja, ukishindwa kuzingatia haya itagharimu muda na fedha zako,” amesema Mnyalape.

Mwakilishi wa benki ya CRDB, Dennis Kayanda aliwasisitiza wajasirmali hao kuzingatia utoaji wa ushuru wa ardhi, akisema inaweza kuwaathiri katika uchukuaji wa mikopo katika benki za biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maziwa Shambani ambaye ni mnufaika wa mafunzo hayo, Victor Mfinanga amesema yamemsaidia kuelewa mbinu za kimfumo na teknolojia za uendeshahji wa biashara zake.

Mafunzo hayo yaliyoudhuriwa na wajasiriamali kutoka mkoani Morogoro, yalihusisha wadau zikiwemo benki za CRDB, NMB NBC, Azania,  Benki ya Afrika pamoja na Chama Cha Biashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA).

Chanzo: mwananchi.co.tz