Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajasiriamali 260 kushiriki Maonyesho ya Fahari ya Geita

Picha Wajasiriamali Data Wajasiriamali 260 kushiriki Maonyesho ya Fahari ya Geita

Fri, 19 May 2023 Chanzo: Mwananchi

Wajasiriamali zaidi ya 250 kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki maonyesho ya nne ya Fahari ya Geita yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 26, 2023 hadi Juni 4, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya maonyesho hayo yanayofanyika mjini Geita kila mwaka, Raphael Siyantemi amesema hadi sasa, wajasiriamali 260 kutoka nchi za Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania wamethibitisha kushiriki maonyesho ya mwaka huu.

Maonyesho hayo yanayokutanisha washiriki kutoka taasisi na mashirika ya umma, kampuni na watu binafsi yanalenga kuwakutanisha na kutoa fursa ya uwekezaji na biashara kwa wadau kutoka sekta ya Kilimo, mifugo na Uvuvi, madini na biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 19, 2023, Siyantemi ambae pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya African Creative amesema maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi Mei 26, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella na kufungwa Juni 4, 2023 na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji.

Amesema Mkoa wa Geita uliojaaliwa utajiri wa madini ya dhahabu utatumia maonyesho hayo kutangaza fursa za uwekezaji na biashara katika sekta ya madini, utalii, kilimo, uvuvi, mifugo na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na mifugo.

‘’Geita pia tunazo fursa za uwekezaji katika biashara ya huduma, hasa katika sekta ya utalii,’’ amesema Siyantemi

Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo nchini (Sido) Mkoa wa Geita, Nina Nchimbi amewataka wajasiriamali kutoka ndani na nje ya mkoa huo kutumia maonyesho hayo kama fursa ya kujitangaza shughuli zao na kupata wawekezaji watakaoongeza mitaji, ujuzi na teknoloji.

Amewashauri wajasiriamali hao kuwekeza katika utafiti kujua mahitaji ya soko ili wazalishe bidhaa zinazohitajika sokoni.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi amesema pamoja na kufanya biashara kwa kuuza bidhaa na huduma, wajasiriamali watakaoshiriki wajikite katika kujifunza mbinu mpya kutoka kwa wenzao ili kuongeza tija katika shughuli zao, hasa kwenye eneo la kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

Chanzo: Mwananchi