Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajasiliamali kukopeshwa Tsh bilioni 48

Makipo Ya Watoa Huduma Huzingatia Masharti Ya Mikataba   Mwigulu Dkt. Mwigulu Nchemba

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema, kwa mwaka 2024, Mfuko wa Huduma Ndogo za Fedha – SELF unatarajia kutoa mikopo yenye masharti nafuu ya shilingi bilioni 48 kwa Wajasiriamali 48,000.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka 2024/2025, Bungeni Jijini Dodoma leo June 04,2024, Mwigulu amesema; “Mfuko huo unatarajia kukuza faida kabla ya kodi hadi shilingi bilioni 3.28 kutoka shilingi bilioni 1.89 mwaka 2023, kukuza mtaji hadi shilingi bilioni 65.48 kutoka shilingi bilioni 61.14 mwaka 2023”

“Kuongeza idadi ya Wateja hadi 48,000 kutoka wateja 37,024 mwaka 2023, kukusanya marejesho ya mikopo iliyo nje ya mizania ya mfuko shilingi bilioni 2 na mikopo iliyo katika mizania shilingi bilioni 48.53 na kukusanya mapato ya jumla ya shilingi bilioni 11.03.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live