Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waholanzi kuwekeza bil 132/- kwenye mkonge

A862172a7e3360d2b91c049281f2fe5e Waholanzi kuwekeza bil 132/- kwenye mkonge

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPUNI ya Mkonge ya Grosso (Grosso Sisal Company Limited) inakusudia kuwekeza zaidi ya Sh bilioni 132 kwa ajili ya usindikaji wa zao la mkonge mkoani Tanga na kupata bidhaa mbalimbali ya zao hilo.

Kampuni hiyo yenye makao makuu nchini Uholanzi ipo nchini kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo hususani zao la mkonge.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Grosso Sisal Company Limited, Nuradin Osman ambaye amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kama njia mojawapo ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao yaliyosahaulika hapa nchini.

“Kiasi cha fedha cha dola milioni 5.7 (Sh132.17 bilioni) kitaingizwa kwenye ukuzaji wa zao la mkonge kwa kuanzisha viwanda vya kuchakata mkonge vitakavyoongeza thamani. Ukuzaji wa sekta ya mkonge nchini ndiyo lengo kuu la kampuni kwa sasa lakini pia kuwafaidisha wakulima wa chini ambao ndio wazalishaji wakuu…

“bado kuna pengo kubwa la uzalishaji, teknolojia ni hafifu na faida ndogo kwa wakulima na wawekezaji na wadau wenmgine katika sekta hiyo. Kutokana na hali hiyo sekta hiyo haiwezi kuvutia soko la kimataifa jambo linaloathiri uchumi wa nchi,” alisema.

Aliongeza kuwa, “Mnyororo wa thamani wa zao hilo hautumiki ipasavyo kwani ni asilimia mbili tu ya nyuzi zinazopatikana na asilimia 98 inaachwa wakati inaweza kusaidia kuzalisha sukari na hata vileo,” alisema Osman.

Akiainisha kuhusu uwekezaji wake, Osman alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya uwekezaji wataanza na dola 700,000 (Sh bilioni 1.6) kuimarisha mfumo wa huduma kwa wateja kwa kuunganisha wazalishaji ambao ni wakulima na wateja duniani kote.

Katika awamu ya pili alisema kampuni itawekeza dola milioni tano kutoka mwaka wa tatu hadi mwaka wa tano wa uwekezaji utakuwa ni wa kuongeza thamani katika sekta.

Kwa kukadiria, Osman alisema kuwa uwekezaji huyo kwa kuanzia utawanufaisha zaidi ya wakulima 3,000 wa mkonge mkoani Tanga.

Chanzo: habarileo.co.tz