Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahoji kasi ujenzi barabara Tamco - Mapinga

Lami Barabaraaaa Wahoji kasi ujenzi barabara Tamco - Mapinga

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bagamoyo. Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, waitaka Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya Tamco – Mapinga, inayojengwa kwa kiwango cha lami ili kuwaondolea adha ya gharama kubwa na muda wanaopoteza safarini.

Wameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 30,2023 katika mkutano uliofanyika Bagamoyo, ukihusisha wananchi, watendaji wa ngazi mbalimbali, na madiwani ambao umeongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Halina Okashi.

Kwa mujibu wa wakazi hao kero wanazokumbana nazo kwa sasa ni pamoja na kutumia zaidi ya saa mbili barabarani, gharama kubwa ya nauli (Sh3,500) kutoka Bagamoyo hadi Kibaha – Loliondo ambalo ni eneo maarufu kwa biashara mbalimbali mkoani humo.

"Hii barabara ina umuhimu mkubwa sana kiuchumi, kama itakamilika kwa wakati, itarahisisha shughuli za biashara na uchumi lakini pia itasaidia ulinzi wa afya afya zetu, kwani hatutatumia muda barabarani,” amesema Katalina Samuel ambaye ni mfanyabiashara wa samaki.

Kwa upande wake Mohamed Habibu ametaka halmashauri hiyo kuiboresha stendi ya mabasi makubwa ili iweze kuongzea mapato kupitia tozo mbalimbali.

"Hata stendi ya mabasi ni vema ikaangaliwa ili iwe imara na mabasi yote yawe yanaingia na kulipia ushuru wa huduma, mapato yataongezeka tofauti na ilivyo sasa ambapo mapato ni kiduchu na mengine yanapotelea hewani bila kuingia kwenye mfuko wa halmashauri,” amesema Habibu.

Akijibu moja ya maswali yaliyohusu ujenzi wa barabara ya Makofia – Mlandizi pamoja na ile ya Tamco – Mapinga, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharamí Mkenge amesema, “.Hivi sasa barabara hizo ziko kwenye hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kuanza na nyingine kuendelea.

Kuhusu stendi ya mabasi, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohamed Usinga amesema wametenga eneo lenye ukubwa wa heka 19 na tayari andiko la mradi limeshakamilishwa, huku ujenzi ukitarajiwa kugharimu Sh4.8 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live