Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahitimu bora IFM kuajiriwa na chuo

9773 IFM+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kina mpango wa kuajiri vijana watano waliofanya vizuri katika masomo yao katika kozi ya usimamizi wa bima.

Wanafunzi hao ni wale waliomaliza katika miaka tofauti huku wengine wakiwa tayari waliwahi kujitolea katika mashirika mbalimbali ya umma na binafsi pamoja na chuoni hapo.

Hayo yamesemwa leo Agosti 2 na Mkuu wa chuo cha IFM, Profesa Tadeo Satta wakati akikabidhi zawadi za ya cheti na Sh2.2 milioni kwa mwanafunzi bora wa shahada ya kwanza katika mwaka wa masomo 2017/2018, Novath Valerian aliyemaliza kozi ya Uhasibu.

Profesa Satta amesema kuajiriwa kwa vijana hao kutatoa motisha kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika masomo yao ili waweze kupata fursa za ajira chuoni hapo na katika mashirika mbalimbali.

"Kama chuo huwa tunawapa zawadi wanafunzi wetu wanapofanya vizuri  katika masomo yao lakini pia huwa tunawapa nafasi ya kufanya kazi kwa vitendo  katika vyuo vyetu kupitia kozi walizozisomea na baadae tunapopewa kibali cha ajira huwa tunawaajiri kama wakiwa tayari," amesema Profesa Satta.

Amesema wameamua kuwaajiri vijana waliofanya vizuri katika kozi ya usimamizi wa bima katika tawi jipya la Mwanza ili kuongeza ufanisi na utendaji wa chuo hicho.

 Naye mwanafunzi bora, Valerian amesema fedha aliyopewa ataitumia katika kuanzisha biashara ili  kujiwekea kumbukumbu ya kile alichokivuna katika masomo yake.

"Najiendeleza kimasomo ili niweze kuwa na ujuzi wa kutosha na nikipata nafasi ya kufundisha itakuwa ni fursa kwangu ya kuwapatia wenzangu ujuzi na maarifa niliyonayo," amesema Valerian.

Chanzo: mwananchi.co.tz