Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahasibu nchini Tanzania kutoa darasa kwa wakulima, wafanyabiashara

81247 Wahasibu+pic Wahasibu nchini Tanzania kutoa darasa kwa wakulima, wafanyabiashara

Tue, 22 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimeandaa onyesho la ‘dawati la Mhasibu’ katika mikoa mitano kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara wakubwa na kati, wakulima, wavuvi, wafugaji, mafundi na waajiriwa.

Katika maonyesho hayo, makundi hayo yatapata fursa ya kukutana na wahasibu, wakaguzi wa hesabu, washauri wa kodi, masuala ya biashara na wakala mbalimbali wa Serikali.

Maonyesho hayo yatakayofanyika Novemba 2, 2019 yatafanyika Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya na manispaa ya Moshi ambako kutakuwa na washiriki wa kanda tano ya mashariki, kati, kaskazini, kanda ya ziwa na kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Oktoba 22, 2019 makamu mwenyekiti wa TAA, Odemari Rushita amesema lengo la maonyesho hayo ni kuwajengea uwezo wa kujua umuhimu wa kufanya mahesabu.

“Tunataka kusaidia Watanzania unaotegemea shughuli hizi wafanye uzalishaji wenye tija na kuwaondolea dhana ya kuwa kuajiri watu wa kada kama yetu ni gharama. Tunataka kuona wanakuza biashara zao, watumie wataalamu wa hesabu katika kuendesha shughuli zao,” amesema.

 

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz