Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahandisi wampewa mwezi mmoja kuwa na leseni

Bashungwa Awasili Morogoro, Atekeleza Agizo La Rais Samia Kufika Pasipofikika Wahandisi wampewa mwezi mmoja kuwa na leseni

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewataka wahandisi na washauri rlekezi wote nchini kuhakikisha wanakuwa na leseni za uhandisi zinazowapa uhalali wa kufanya kazi za kihandisi nchini ifikapo Machi 31, 2024.

Amesema hayo leo Dar es Salaam katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 21 ya Mpango wa Mafunzo kwa Vitendo kwa Wahandisi Wahitimu (SEAP) na uzinduzi wa ufadhili kwa wahandisi wa kike, unaofadhiliwa na Serikali ya Norway.

Bashungwa ameipongeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kwa kuanzisha utaratibu wa kuwaapisha wahandisi wataalamu wote kwani taaluma hiyo ni nyeti sana kwa uchumi wa nchi, usalama wa mazingira, na maisha ya watu na mali zao.

Aidha, amesema mpango huo wa SEAP umekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza ujuzi wa wahandisi wahitimu nchini kwa kuwawezesha kupata uzoefu wa vitendo unaohitajika katika soko la ajira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live