Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafundishwa viwango katika mafuta ya mawese

A94a35f70c519c0e57008e3c0d7bcc53 Wafundishwa viwango katika mafuta ya mawese

Wed, 9 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ILI kuongeza thamani ya mafuta ya mawese, wadau 12,200 wakiwemo wakulima, wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa mafuta hayo mkoani Kigoma, wamepatiwa mafunzo ya uzalishaji, usindikaji na utunzaji kwa kuzingatia viwango na vifungashio bora.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo katika ukumbi wa chuo cha waganga Kigoma Mjini mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga, alisema ili mafuta ya kula yawe bora ni lazima kuzingatia kanuni bora za kilimo, usindikaji na afya.

Msasalaga alisema wazalishaji wengi wa mawese na mafuta mengine ya kula wamekuwa wakitumia njia za asili ambazo hazizingatii ubora na usalama wa mafuta hayo na hivyo kusababisha madhara kwa walaji.

Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi wa TBS, Rodney Alananga, aliwataka wasindikaji kufuata taratibu za uthibitishaji ubora wa mafuta hayo kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza masoko ya ndani na nje ya nchi lakini pia kutalinda afya na usalama wa walaji.

Akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye Kata ya Ngaruka wilayani Katavi, Meneja Mafunzo na Utafiti wa TBS, Hamis Sudi, alisema serikali inathamini mchango wa wajasiriamali katika kukuza uchumi wa nchi.

Alisema kutokana na umuhimu huo, serikali itaendelea kutoa mafunzo hayo nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha kuwa wazalishaji wa mafuta ya kula nchini wanazalisha bidhaa hiyo kwa kuzingatia viwango vya kitaifa vilivyopo.

Ofisa Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Festo Kapela, alisema kuwa zaidi ya asilimia 50 ya mafuta ya kula yanayotumika nchini huagizwa nje ya nchi kwa gharama kubwa na kwamba ikiwa mafuta ya mawese yatapewa ubora, serikali itaweza kuokoa gharama kubwa.

Chanzo: habarileo.co.tz