Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafugaji wa nyuki waomba ulinzi wa misitu

MKUPA Wafugaji wa nyuki waomba ulinzi wa misitu

Sat, 29 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafugaji wa Nyuki Wilayani Chato wameiomba serikali iweze kuongeza Ulinzi kwenye misitu ya hifadhi ili wavamizi wenye tabia ya kukata na kuchoma misitu waache tabia hiyo na wao wanufaike na zao la Nyuki.

Wafugaji hao wametoa malalamiko hayo wakati wanakabidhiwa mizinga ya Nyuki 125 na shirika la hifadhi ya Taifa kupitia hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambapo wameeleza kuwa mizinga yao imekuwa ikiharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Martha Mkupasi akiwataka wafugaji hao kuacha kuwafumbia macho wale wote wanaohusika na uharibifu wa misitu ili wakipatikana wachukuliwe hatua kali za kisheria.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live