Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi sekta ya mifugo Tixon Nzunda, amewataka maafisa ugani pamoja na wafugaji kote nchini kusajiliwa katika mfumo wa kielekroniki ili kufuatilia utendaji wao wa kazi na uwajibikaji uendane na wakati pamoja na kuboresha uzalishaji wa mifugo nchini.
Katika mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa ugani kutoka mikoa ya nyanda za Juu Kusini, yaliyofanyika Mjini Makambo, Katibu Mkuu huyo amesema licha ya wizara kuwasajili maafisa ugani katika mfumo wa kielektroniki lakini serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inajenga majosho 260 ili kuhakikisha wafugaji wanafuga kwa tija.
Kwa upande wao maafisa ugani wa nyanda hizo wamesema mkakati ambao umeletwa na serikali uanenda kuimarisha idara hiyo ya mifugo ambayo ilikuwa imesahaulika.