Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafugaji na kitanzi utunzaji miundombinu

467d20f103f08d0537a9af64f2c25853 Wafugaji na kitanzi utunzaji miundombinu

Sun, 24 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Sahili Geraruma amewataka wafugaji wilayani Bukombe mkoani Geita kuheshimu na kuthamini miundombinu ya barabara na kuacha kupitisha mifugo yao.

Geraruma ametoa maelekezo hayo baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara mpya ya Nampalahala-Idoselo, yenye urefu wa kilomita sita katika mundelezo wa mbio za mwenge kitaifa zinazoendelea mkoani Geita.

Amesema upitishaji wa mifugo hasa ng’ombe katikati ya barabara ni miongoni mwa sababu kubwa inayoleta uharibifu wa barabara, hivyo ni lazima wafugaji wabadilike na kuchukua hatua kwa maendeleo ya taifa.

Amesema serikali inawekeza fedha nyingi kila mwaka kuhakikisha ukarabati wa barabara, hivyo ni lazima kila mmoja kwa nafasi yake achukue hatua kudhibiti uharibifu wa aina yeyote na miundombinu iweze kudumu.

Mkimbiza Mwenge kitaifa, Emmanuel Chacha amewataka wahandisi wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), kuongeza nguvu katika usimamiaji wa miradi badala ya kutumia muda mwingi kupiga simu.

“TARURA nendeni ‘site’, acheni kukaa ofisini mnakuwa mnapiga simu tu, tunataka tuone mnasimamia hatua kwa hatua, toka barabara inaanza mpaka inakamilika na ikikamilika iwe bora ianze kutumika,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live