Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabishara Waelekezwa Kushusha Bei ya Vifaa vya Ujenzi

Ujenziii Wafanyabishara Waelekezwa Kushusha Bei ya Vifaa vya Ujenzi

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema tathmini iliyofanyika imebaini ongezeko holela la bei ya vifaa vya ujenzi hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Ashatu Kijaji amesema wamebaini ongezeko limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

Ameelekeza Wazalishaji na Wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela. Mamlaka za Udhibiti zimeagizwa kuchukua hatua dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live