Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabisahara wa Tanzania na Congo kukutana

Screenshot 20220226 130257 Facebook Wafanyabisahara wa Tanzania na Congo kukutana

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Tanzania na Kongo zimepanga kuandaa mkutano mkubwa wa pamoja kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa Congo DR ili kuzungumzia mwelekeo wa kibiashara.11

Amesema kuwa mkutano huo ambao utajadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabiashara wa nchi mbili hizo na namna ya kuzitatua utasaidi kuchochea uchumi wa kitaifa na wa mtu mmoja mmoja.

Amesema hayo jana (Februari 25, 2022) baada ya mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sama Lukonde yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu huyo jijini Kinshasa.

“Tuna fursa katika ziwa Tanganyika ambapo Tanzania tumejenga bandari tano muhimu zinaoweza kutumiwa na DRC, pia tuna barabara tunayoitumia kutoka Tunduma kwenda Kaprimposhi-Kasumbalesa, tunataka kubadilisha “route” ipite kwenye daraja la Kasenga barabara ambayo ni fupi sana inapunguza zaidi ya kilomita 2000 kwenda na kurudi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live