Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara watatu kizimbani kwa kuchezesha upatu

48612 Upatu+pic

Tue, 26 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Wafanyabiashara watatu wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kuendesha biashara ya upatu na kujipatia kiasi cha Sh330 milioni.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 22 ya 2019 ni Agnes Lobulu (49) mkazi wa ubungo, Frorian Mjwahuzi (32) mkazi wa Mbagala na George Ruhara (55) raia wa Kenya.

Akisoma hati ya mashtaka jana Jumatatu Machi 25,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando wakili wa Serikali, Jenipher Masue alidai katika shtaka la kwanza washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kula njama na kutenda kosa kinyume na sheria.

Katika shtaka la pili alidai washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kufanya biashara ya upatu kinyume na sheria ambapo inadaiwa kati ya Januari 1, na Machi 15, 2019 katika Jiji la Dar es salaam na maeneo mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliendesha biashara ya upatu na kujipatia Sh330 milioni.

Katika shtaka la tatu washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutakatisha fedha kinyume na sheria.

Inadaiwa kati ya Januari 1 na Machi 15,2019 ndani ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ndani ya Tanzania washtakiwa hao kwa pamoja walitakatisha kiasi cha Sh330 milioni wakijua kwamba fedha hizo zimepatikana kwa njia isiyo halali na ni zao la upatu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Wakili Masue alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba Mahakama ipange tarehe nyingine ambapo Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 4, 2019 itakapotajwa tena na washtakiwa wote wamepelekwa rumande.



Chanzo: mwananchi.co.tz