Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara watafiti nchi tisa kukutana Dar

9719 KONGAMANO+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), imeandaa kongamano la siku mbili litakalowakutanisha watafiti kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Kongamano hilo la 18 la kimataifa la maendeleo ya ujasiriamali na biashara ndogo na za kati Afrika, litawakutanisha washiriki kutoka nchi tisa.

Akizungumza leo Agosti 2, 2018 mkuu wa shule hiyo, Dk Ulingeta Mbamba amesema lengo la kongamano hilo ni kuangalia maandiko na tafiti mbalimbali jinsi zinavyowasaidia  wajasirimali na watunga sera kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi jumuishi.

Amesema zaidi ya mada 46 zitawasilishwa na kujadiliwa katika kongamano hilo litakalofanyika Agosti 9 hadi 10 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema mada kuu katika kongamano hilo ni ujasiriamali kwa ujumla, kilimo biashara na uchumi jumuishi.

"Kuna faida nyingi za uwepo wa kongamano hili ikiwamo kujadili mikwamo, changamoto na kutafuta suluhisho. Inawezekana wakati watunga sera kwa maana ya Serikali wakidhani changamoto ya wafanyabiashara ni mitaji wafanyabiashara wana changamoto ya masoko,” amesema Dk Mbamba.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz