Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara washauriwa kuweka nembo

A95DBEB7 3665 48C3 87E8 8D85E962EC99.png Wafanyabiashara washauriwa kuweka nembo

Sun, 21 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKALA wa vipimo nchini (WMA) mkoani Shinyang, wamewashauri wafanyabiashara kuweka nembo kwenye vifungashio, ili kutambulika kisheria kwa usalama wao na bidhaa zao.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Ofisa Vipimo Mkoa, Happiness Saronge, wakati akizungumza na wafanyabiashara wa mchele eneo la Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga kuadhimisha Siku ya Vipimo duniani, yenye kauli vipimo vinavyotumika kwenye mfumo wa chakula duniani.

Saronge amesema wanatoa elimu ya vifungashio, wafanyabiashara wanatakiwa wawe na nembo, ili ijulikane imetengenezwa lini, muda wa kuisha matumizi yake na vipimo vilivyomo kama ni sahihi.

“Wafanyabiashara kila mwaka wanatakiwa kukaguliwa mizani zao, lengo ni kuona kama inapunja mteja au kujipunja na wenye mizani mipya wahakikishe inakaguliwa, wapo wanaofanya udanganyifu katika kufungasha,”amesema Saronge.

Amewataka wanaofungasha waweke pia majina yao kwa kutumia mashine sio kwa kuandika na kalamu, hilo ni kosa kisheria.

Amesema marekebisho ya mzani yanafanyika kwa gharama kidogo kwa kutofautisha aina ya mizani aliyonayo mfanyabiashara.

Baadhi ya wafanyabiadhara waliohudhuria utolewaji wa elimu hiyo, akiwemo Joel Albert, amesema wakulima vijijini wao wenyewe wanapenda kutumia vipimo vya ndoo, wakienda na mizani wanaikataa kwa kudai hawaiamini.

Ezeckiel Mabala amesema wao ni wafanyabiashara wanaouza kwa rejareja, kuweka nembo itakuwa ni ngumu, kwa sababu hawatumii vifungashio, mteja anakuja moja kwa moja mashine kuchukua mchele akiwa na kifungashio chake.

Wafanyabiashara hao waliomba Wakala wa vipimo inapofika wakati wa ukaguzi mizani waende moja kwa moja kwenye maeneo yao, siyo kwenye ofisi za watendaji wa kata unakuwa ni usumbufu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live