Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara washauriwa kuchangamkia Fursa

55a09657d407e6e813e91d1db7a96f91 Wafanyabiashara washauriwa kuchangamkia Fursa

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAFANYABIASHARA Wakubwa wa kati na wadogo mkoani Mwanza wameshauriwa kuchangamukia fursa kwa kujiunga na mifuko ya uwekezaji nchini (UTT-AMIS) ili waweze kunufaika na faida mbalimbali ikiwemo kupatiwa ushauri na elimu ya uwekezaji pamoja na kufungua akaunti na kuwekeza kwenye mifuko hiyo.

Rai hiyo ilitolewa jana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wa Mwanza, Emmanuel Tutuba wakati akizindua rasmi ofisi za UTT AMIS mkoani hapa, ambapo alisisitiza uzinduzi wa ofisi hizo utakuwa na manufaa kwa wafanyabiashara na vyama vya ushirika.

Tutuba alisema mbali na wafanyabiashra pia uwepo wa UTT AMIS utawasaidia wastaafu mkoani hapa kuwekeza na kupata riba ama gawio na pengine kupatiwa elimu ya uwekezaji na kuumaliza ugonjwa wa wastaafu kufirisika baada ya kupokea mafao yao kutokana na kujiingiza katika biashara wasizokuwa na uzoefu nazo.

Aidha alipongeza ujio wa ofisi hizo mkoani hapa kwa kuwa utasaidia kukua kwa uchumi kwani Mwanza ni kitovu cha uchumi na biashara mikoa ya kanda ya ziwa na kwa nchi za Afrika Mashariki hivyo ni vyema pia wakazi wa Mwanza wasibaki nyuma kujiunga na mfuko huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya UTT AMIS, Issa Mohamed alisema hadi sasa kampuni hiyo imeshaanzisha na inasimamia mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni umoja, wekeza maisha, watoto, jikimu, ukwasi na hati fungani ambapo wakazi wa mwanza na watanzania kwa ujumla wanaweza kujiunga na kufaidika nayo.

Mohamed aliwaomba watanzania kutokuwa na shaka iwapo watahitaji kujiunga na kuwekeza UTT AMIS kwa kuwa kampuni hiyo ni ya serikali na inafanya kazi chini ya wizara ya fedha na mipango na inatekeleza majukumu yake kulingana na sheria ya masoko ya mitaji na dhamana ya mwaka 1994 na marekebisho yake pamoja na kanuni za mfuko ya uwekezaji wa pamoja za mwaka 1997.

Chanzo: habarileo.co.tz