Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wapongeza utaratibu benki kukutana nao

6760713968dfa4f39fe3f82e1f8ea159 Wafanyabiashara wapongeza utaratibu benki kukutana nao

Mon, 9 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UMOJA wa Wafanyabisha Wateja wa Benki ya NMB katika mikoa ya Shinyanga, Geita na Tabora, umeipongeza benki hiyo kwa kuweka utaratibu wa kukutana nao na kuwasikiliza.

Wafanyabishara hao wamesema kupitia utaratibu huo,wamepata fursa zaidi kuelezea changamoto zinazowakabili katika biashara zao na kutoa maoni kuhusu uboreshwaji wa huduma.

Wafanyabiashara hao wakiwemo wajasiriamali kutoka wilaya za Kahama mkoa wa Shinyanga, Mbogwe mkoani Geita na Uyui katika Mkoa wa Tabora, walisema hayo mwishoni mwa wiki baada ya kukutanishwa na benki hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wa umoja huo, Mwenyekiti wa Klabu ya Wafanyabiashara kutoka Wilaya ya Kahama, Azan Said alisema utaratibu huo wa NMB unawapa nguvu ya kuendelea kufanya kazi na benki hiyo.

Saidi alisema kupitia utaratibu huo ambao huwasilisha changamoto zao, maoni na ushauri umewafanya kuwa imara katika biashara zao na kusababisha wawe warejeshaji wazuri wa mikopo.

Mfanyabiashara Haji Nasor alisema wanaridhishwa na uboreshaji wa huduma unaofanywa na NMB na kuwasisitiza wafanyabishara wengine kuchangamkia fursa zitolewazo na benki hiyo.

“Kwa muda mrefu NMB imekuwa mkombozi kwetu. Kupitia utaratibu huu wa kukutana, tumenufaika kwa kiwango kikubwa kwani huduma nyingi zimeboreshwa hasa katika mikopo ya kibiashara,” alisema Nasor.

Katika Kongamano hilo, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi, Sospeter Magese aliwahakikishia wafanyabishara hao kuwa benki hiyo itaendelea kuweka mazingira mazuri zaidi kuwawezesha kiuchumi ili kwenda na wakati na ukuaji wa uchumi wa taifa.

Magesse alisema wamekuwa na utaratibu wa kukaa na wateja wao kila mwaka ili kuboresha huduma na kuwakuza kiuchumi.

“NMB inamilikiwa na wateja kwa hisa zenu pamoja na serikali na inahakikisha huduma za kibenki zinawafikia popote mlipo kupitia mawakala wetu na kwa umuhimu huo ndiyo maana inaendelea kuyafanyia kazi mawazo na ushauri wao,” alisema Magesse.

Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara, Loelia Kibassa, aliwataka wanajamii kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotolewa na benki ya NMB ikiwamo mikopo inayoanzia Sh 500,000 mpaka Sh bilioni tano na kurejesha kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kuwawekea mazingira rafiki wafanyabiashara iliwafanikiwe zaidi kiuchumi kupitia mikopo.

Macha aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali hao kuwa waaminifu kwa taasisi za fedha na benki zinazowapatia mikopo kwa kurejesha kwa wakati.

Chanzo: habarileo.co.tz