Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara waonywa kupandisha bei wakati wa Sikukuu

Wafanyabiashara Waonywa Kupandisha Bei Wakati Wa Sikukuu.jpeg Wafanyabiashara waonywa kupandisha bei wakati wa Sikukuu

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ametoa rai kwa wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali nchini kuwa waadilifu katika kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kutokupandisha bei za bidhaa bali kuhakikisha wanazingatia ushindani wa haki katika biashara zao.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Desemba 15, 2022 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia mwenendo wa bei za bidhaa muhimu nchini kwa Desemba 2022 ambapo amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayejaribu kupandisha bei za bodhaa kiholela ili kuumiza Wananchi.

Amesema, Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kudhibiti upandaji wa bei ikiwemo kutoa ruzuku katika mafuta ya petroli na mbolea hivyo iko tayari kuwachukulia hatua watakaopandisha au waliopandisha bei ya vyakula bila ya kiholela kwa kutumia sheria za ushindani ili kiwalinda walaji na wafanyabiashara wenyewe.

Kuhusu bei za vyakula amesema mwenendo umeendelea kupanda kidogo katika baadhi ya Mikoa na kushuka katika baadhi ya Mikoa huku bei ya Vifaa vya Ujenzi ikionyesha kuwa ya uhimilivu.

Aidha amesema bei za bidhaa zimeendelea kutofautiana katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo sehemu nyingi bei za vyakula zimeendelea kupanda kutokana na kupungua kwa Uzalishaji katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021 hadi 2022 kutokana na hali ya hewa isiyoridhisha hapa nchini na nchi za jirani na kupanda kwa bei ya petrol duniani, UVIKO 19 na vita vya Ukraine na Urusi.

Kutokana na umuhimu huo amewahimiza maofisa biashara nchini kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu mwenendo wa bei kwenye maeneo wanayosimamia pamoja na kukusanya Taarifa za bei na kuziwasilisha kwa wakati Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

"Lengo la Wizara ya Viwanda Biashara na uwekezaji ni kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali ili kuwawezesha Walaji, wadau pamoja na wazalishaji kujua taarifa sahihi za bei za bidhaa ambazo wanatumia,"amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live