Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara waombwa kujiunga na mifuko ya uwekezaji

7166b6d47791b80490069eb947fe1883 Wafanyabiashara waombwa kujiunga na mifuko ya uwekezaji

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAFANYABIASHARA mkoani Mwanza wameshauriwa kuchangamkia fursa kwa kujiunga na mifuko ya uwekezaji nchini (UTT-AMIS) ili waweze kunufaika na faida mbalimbali ikiwemo kupatiwa ushauri na elimu ya uwekezaji pamoja na kufungua akaunti na kuwekeza kwenye mifuko hiyo.

Rai hiyo ilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Tutuba wakati akizindua rasmi ofisi za UTT AMIS mkoani hapa na kusisitiza uzinduzi wa ofisi hizo utakuwa na manufaa kwa wafanyabiashara na vyama vya ushirika.

Tutuba alisema mbali na wafanyabiashra pia uwepo wa UTT AMIS utawasaidia wastaafu mkoani humo kuwekeza na kupata riba ama gawio na pengine kupatiwa elimu ya uwekezaji na kuumaliza ugonjwa wa wastaafu kufirisika baada ya kupokea mafao yao kutokana na kujiingiza katika biashara wasizokuwa na uzoefu nazo.

Aidha alipongeza ujio wa ofisi hizo mkoani humo kwa kuwa utasaidia kukua kwa uchumi kwani Mwanza ni kitovu cha uchumi na biashara mikoa ya kanda ya ziwa na kwa nchi za Afrika Mashariki hivyo ni vyema pia wakazi wa Mwanza wasibaki nyuma kujiunga na mfuko huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya UTT AMIS, Issa Mohamed alisema hadi sasa kampuni hiyo imeshaanzisha na inasimamia mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni umoja, wekeza maisha, watoto, jikimu, ukwasi na hati fungani na kuwa wakazi wa Mwanza na watanzania kwa ujumla wanaweza kujiunga na kufaidika nayo.

Chanzo: habarileo.co.tz