Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara, wanunuzi mbaroni Matumizi ya risiti

Pingu 1?fit=1024%2C682 Waingia matatani na TRA kwa kutotoa risiti

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha imewakamata na kuwatoza faini Watu 44 kwa kusahau kuchukua risiti kwenye maduka mbalimbali baada ya kufanya manunuzi huku Wafanyabiashara 30 nao wakikamatwa kwa kutokutoa risiti.

Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Arusha Bashiru Kahenaki amesema;

"Mara nyingi tulikua tukiwafata Wauzaji peke yake lakini sasa hivi tunawafata mpaka Wateja hivyo ni Muuzaji na Mnunuzi wote watekeleze wajibu wao wa kisheria, zoezi linaendelea vizuri na kiasi kikubwa tumekuta Watu wanatekeleza ila wale wachache wasiofata kanuni tumewaadhibu"

Kwa mujibu wa sheria za kodi Mteja anaenunua bidhaa yoyote dukani bila kudai risiti anatozwa faini ya kuanzia elfu 30 mpaka milioni moja na nusu huku Muuza duka asietoa risiti akitozwa milioni tatu mpaka milioni nne na laki tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live