Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara walia na kodi za mapato, upangishaji

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kodi ya mapato na ile ya zuio la upangishaji zimetajwa na wafanyabiashara kuwa zinawaumiza katika shughuli zao za kila siku na kuiomba mamlaka husika kuangalia namna ya kuzikusanya.

Hayo wameyasema leo Ijumaa Mei 17, 2019 ikiwa ni uhitimishaji wa Wiki ya elimu kwa mlipa kodi iliyokuwa ikitolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumzia kodi ya zuio la upangishaji, mmoja wa wafanyabiashara katika soko la Tandika, Hawa Abdull amesema asilimia 10 wanayotozwa na TRA kama zuio la kodi ya upangishwaji katika maeneo yao ya kufanyia biashara, siyo halali wao kuilipa lakini pia ni ngumu kwa mmiliki kukubali kukatwa fedha hiyo katika kodi anayotakiwa kupewa.

“Ni suala gumu mtu akupangishe halafu umwambie labda Sh150,000 ambayo ni asilimia 10 ya kodi yake unaipeleka TRA, unadhani atakuelewa, labda kama na wewe hautaki kufanya biashara,” amesema Hawa.

Jumanne Mahundi amesema makadirio ya kodi yanayofanywa na TRA yasiwe chanzo cha kuwaumiza na kuwarudisha nyuma katika ufanyaji wa biashara.

 

Pia Soma

“Basi tukifanyiwa makadirio yaendane na kile tunachokipata siyo ukifanyiwa makadirio yakaribie kuzidi mtaji wako yanatuumiza,” amesema Mahundi.

Ofisa Mwandamizi wa Kodi katika wilaya ya Temeke, Bakari Mlandula amesema kodi hizo zimekuwa zikilalamikiwa sana na ili kuondoa malalamiko hayo, wanajitahidi kutoa elimu kwa wamiliki wa nyumba na biashara.

“Hii asilimia 10 ya Kodi ya zuio katika upangishaji inatakiwa kulipwa na mmiliki wa nyumba baada ya kulipwa fedha kutoka kwa mpangaji.

“Sasa kodi hii imekuwa ikiwaangukia wapangaji kwa sababu wamiliki wa nyumba ni ngumu kuwapata na mara nyingi wanatumia madalali katika upangishaji jambo ambalo linaleta ugumu katika ukusanyaji wake.”

Akizunguzumzia suala la makadirio ya kodi Mlandula amesema changamoto ya utunzaji wa kumbukumbu za mauzo waliyonayo wafanyabiashara imeleta ugumu kwao kujua kama kiasi cha pesa wanachoambiwa ni kikubwa.

“Unaposema makadirio ni makubwa kuliko mauzo yako tuonyeshe uthibitisho wa rekodi ya mauzo yako sasa kama hauna ni ngumu sisi kuamini kama biashara ilikuqa ngumu,” amesema.

 

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz