Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara walia hali ngumu kuelekea Eid

59988 PIC+EID

Tue, 28 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Zikiwa zimesalia siku takriban tisa kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, maandalizi ya Sikukuu ya Eid el Fitr yameanza huku wafanyabiashara wakilalamikia hali ngumu ya biashara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Tandika wamesema hali ya biashara inazidi kuwa mbaya ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.

“Miaka minne iliyopita mwezi 21 kama ilivyo leo nimeshamaliza kuuza na kuagiza tenga mzigo mwingine lakini huu mzigo unaouona hapa nimeuchukua tangu mwezi 15 hadi leo upo na sijui utaisha lini,” anasema Mohammed Mosha mfanyabiashara wa nguo sokoni Tandika.

Alisema licha ya bei kuwa za kawaida lakini bado wateja wanalalamika “mwaka huu sijui kama tutatoboa,”.

Mfanyabiashara wa nguo za watoto sokoni Kariakoo Grace Charles amesema mwaka huu bei za nguo zimepungua kutoka Sh30,000 gauni moja ya mtoto hadi Sh25 000 ili kuendana na hali ya biashara.

“Wakati mwingine tunauza kwa bei ya hasara ili angalau tupate chochote kuliko kukosa kabisa,”ameongeza.

Pia Soma

Mussa Majid mfanyabiashara wa viatu anasema “mimi naona biashara ipo vile vile tu hakuna kilichobadilika maana tukisema mwaka huu hali ya biashara mbaya ni sawa na kusema hakuna kilichobadilika hata mwaka jana ilikuwa hivi hivi, cha msingi namshukuru Mungu maisha yanasonga.”

Makamu Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo (machinga) Kariakoo, Namoto Yusuph amesema bei za bidhaa mwaka huu ni za kawaida ila wateja hakuna kutokana na hali ya uchumi.

Chanzo: mwananchi.co.tz