Wafanyabiashara wanaofanya biashara katika soko la Tengeru wameandamana na na kufunga barabara ya Moshi - Arusha kwa kutumia meza huku wakishinikiza Halmashauri kuondoa meza hizo katika soko hilo wakisema hawakubaliani na utaratibu wa kulipia meza hizo Tsh. elfu nne kwakuwa hawana uwezo wa kulipia.
Vurugu hizo ambazo zilidumu kwa zaidi ya saa nne zilipelekea Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kufika eneo hilo na kuwaomba Wafanyabiashara hao kuondoa meza hizo barabarani na kuwaruhusu Wafanyabiashara kuendelea na kazi huku akiahidi kufanya kikao kingine kitakachowashirikisha.
Tazama video hapa chini;
Wafanyabiashara wanaofanya biashara katika soko la Tengeru wameandamana na na kufunga barabara ya Moshi - Arusha kwa kutumia meza huku wakishinikiza Halmashauri kuondoa meza hizo katika soko hilo wakisema hawakubaliani na utaratibu wa kulipia meza hizo Tsh. elfu nne kwakuwa… pic.twitter.com/jXdmYpUrcy
— millardayo (@millardayo) September 27, 2023