Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa mapambo walalamikia uhaba wa wateja

DB2D4586 B73A 41C6 A66C FABA9864AFAB.jpeg Wafanyabiashara wa mapambo walalamikia uhaba wa wateja

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Wakati msimu wa sikuu za mwisho wa mwaka ukibisha hodi, baadhi ya wafanyabishara wa mapambo ikiwemo maua na miti ya krismasi wamesma kuna dalili ya bidhaa hizo kukosa soko mwaka huu.

Katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo baadhi ya wachuuzi wa miti na mapambo yanayotumika zaidi katika Krismasi waliozungumza na Mwananchi wamelalamika kukosa wateja ikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya siku kuu hiyo.

Seleman Alex ambaye ni mfanyabishara katika soko la Kariakoo amesema tangu amechukua mzigo huo hadi sasa haoni mwelekeo wa kurudisha fedha aliyotumia.

“Nashindwa kuelewa ndiyo hali ngumu ya uchumi au watu bado wana mapambo ya miaka iliyopita. Hatuoni wateja, zamani terehe kama hizi nimeshachukua mzigo mara mbili lakini mwaka huu nimechukua mara moja na bado upo wa kutosha,” amesema Alex.

Hilo limeelezwa pia na Gervas Kayombo ambaye amesema licha ya kuwa bado kuna siku nyingi kabla kufiki krismasi lakini mwenendo wa biashara ya bidhaa hizo hauko vizuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Amesema, “Mambo sio mazuri lakini hebu ngoja tusubiri inawezekana, watu wanashughulika kwanza na mavazi halafu mwishoni ndio watakuja huku kwenye mapambo,” amesema.

Kwa upande wake Omary Mbunda amewasisitza wateja kujitokeza kununua mapambo hayo kwa kuwa yana nafasi kubwa ya kuchangamsha nyumba wakati wa sikukuu.

Katika maeneo mbalimbali miti ya krismasi inauzwa kati ya Sh35, 000 na Sh200, 000 ikitofautiana kwa ubora, urefu na muonekano wa mti husika.

Chanzo: Mwananchi