Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa madini waomba punguzo la kodi

Wanaharakati Wayataka Makampuni Ya Madini Kuwalipa Zaidi Wachimbaji DRC Wafanyabiashara wa madini waomba punguzo la kodi

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wa madini mkoani Geita wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia Tume ya Madini pamoja na halmashauri kupunguza kodi na tozo ambazo ni asilimia 9.3 kwa madini ya dhahabu yanayouzwa katika masoko ya madini nchini.

Wafanyabiashara hao wametoa ombi hilo mbele ya Kamishna Mkuu wa TRA Yusuf Mwenda wakati wa mkutano ulioitishwa na mamlaka hiyo Mjini Geita.

Mwenyekiti wa Soko Kuu la Madini la Geita, George Galoba amesema wafanyabiashara wamekuwa wakitorosha madini na kupeleka nje ya nchi kutokana na kodi katika nchi hizo kuwa chini na hivyo kuiomba Serikali kuangalia namna ya kuboresha sheria za kodi ili Serikali ipate zaidi mapato yatokanayo na madini.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) mkoani Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema kodi na tozo kwa nchi zinazoizunguka Tanzania ziko chini na hivyo kuiomba TRA kuweka mazingira wezeshaji hasa kwa upande wa kodi za madini.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Yusuf Mwenda amesema Serikali itaendelea kuboresha na kubadilisha mifumo ya sheria ili iendande na mazingira ya biashara hapa nchini.

Amesema kama kodi za nchi jirani ni ndogo kuliko za Tanzania basi lazima uboreshaji wa sheria za kodi utazamwe na kurekebishwa ili kuwepo na mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hao wa madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live