Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa mabati wapewa mafunzo TBS

F334d7ae Eafd 4015 Abfe A99d2fd939f4 660x400 Wafanyabiashara wa mabati wapewa mafunzo TBS

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Shirika la Viwango Tanzania TBS limetoa mafunzo kwa wazalishaji, waagizaji, wasambazaji na wadau mbalimbali wa mabati na koili za mabati hapa nchini baada ya Tanzania kukamilisha utaratibu wa kupitisha viwango vya mabati na koili ambavyo ni TZS 353:2020/EAS 11:2019 na TZS 1477:2020/EAS 468:2019 kuwa viwango vya kitaifa pamoja na kiwango Na.1476:2017.

Akizungumza wakati anafungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS Bw.David Ndibalema amesema shirika hilo lilifanya tathimini ambapo ilibaini kuwa yapo mabati na koili za mabati zinazozalishwa na kuaingizwa hapa nchini hazikidhi matakwa ya viwango.

“Mafunzo haya yanalenga kuandaa washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kuzalisha, kuingiza na kusambaza mabati na koili za mabati zinazokidhi matakwa ya viwango”. Ndibalema.

Aidha Ndibalema amesema TBS itaendelea kutilia mkazo kusimamia maswala ya viwango na udhibiti ubora na kwamba biashara zinafanywa katika mifumo inayoeleweka na kukubalika kisheria sambamba na kanuni zinazosimamia mifumo viwango na udhibiti ubora.

Chanzo: millardayo.com