Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa fedha waiomba BoT kufanya upya mapito ya sera hizi..

Fedhapic Wafanyabiashara wa fedha waiomba BoT kufanya upya mapito ya sera

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara ya ubadilishwaji wa fedha za kigeni katika Mpaka wa Tunduma Mkoani songwe wameiomba serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuona namna ya kupitia upya sera ya mitaji kwa wafanyabiashara ambapo wametaka kushushwa kwa gharama za kuanza biashara hiyo hali ambayo imeendelea kuchochoa wafanyabiashara wengi kutorasimisha biashara zao na kuendelea kufanya biashara almaarufu kama Black market.

Katika Mpaka wa Tunduma kumekuwa na kushamiri kwa biashara hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa wafanyabiashara hao huku kilio Chao kikubwa ni kutaka Benki Kuu kupunguza vigezo vya mtaji ambavyo vinamtaka mfanyabiashara anatakiwa kuwa na kianzio cha Millioni 200 na kutakiwa kurasimisha biashara hiyo jambo ambalo limeonekana wafanyabiashara wa kubadilisha fedha kuona kuwa bado gharama ni kubwa na kutoa mapendekezo yao.

Eddy Sanga pamoja na Elija Mwamengo ni baadhi ya Wafanyabiashara waliopo Mpakani Tunduma wametoa mapendekezo yao kwa Serikali kupitia Benki Kuu kuona namna ya kuboresha sera hiyo ili kuwapa fursa wafanyabiashara hao kuwekeza kwenye biashara hiyo.

Wafanyabiashara wameyasema hayo wakati wa kikao kilichoandaliwa na Benki Kuu katika Mji Wa Tunduma cha utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara pamoja na kuwapatia sera mpya ambayo imeletwa ya kuwataka kurasimisha biashara hizo ambazo zimekuwa zikifanyika Mpakani hapo.

Maafisa wa Benki kuu ndugu Abdul Mussa na Inocent Malipa ambao ni Maafisa kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu wameeleza sera hiyo kwa wafanyabiashara pamoja ba kuwapatia elimu juu ya manufaa ya kurasimisha biashara zao ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto ya uwepo wa fedha bandia katika Soko

Chanzo: www.tanzaniaweb.live