Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa Tanznaia na Romania kukutana

Samia Romania Wafanyabiz.jpeg Wafanyabiashara wa Tanznaia na Romania kukutana

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amesema moja kati ya mambo waliyojadiliana na Rais wa Romania Klaus Iohinnis ni kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili na kuiwezesha sekta binafsi katika mataifa hayo kukutana.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya viongozi hao, Rais Samia amesema wamekubaliana kuwa wafanyabiashara kutoka Tanzania waende nchini Romania na wale wa Romania waje Tanzania kujifunza na kufanya biashara kwa pamoja.

"Tumekubaliana kuwa wafanyabiashara baina ya nchi hizo mbili wakutane na wabadilishane uzoefu kwa lengo la kukuza biashara zao na kuwekeza zaidi." - Amesema Rais Samia.

Pia eneo ambalo Tanzania na Romania wamekubaliana kushirikiana ni kukabiliana na majanga ambapo ofisi ya Waziri Mkuu itahusika na usimamizi wa makubaliano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live