Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki wakutana

Kibiashara Uongozi wa Tanzania na Wafanyabiashara wa Uturuki katika picha

Thu, 17 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wa Ndani ya nchi wametakiwa kuendelea kukuza ushirikiano na Wafanyabiashara wengine kutoka nje ya nchi ikiwemo wafanyabiashara kutoka n nchi ya Uturuki ili kuhakikisha Wanakuza na kuongeza thamani ya Mnyoro wa Uchumi wa nchi.

Wito huo Umetolewa na Paul koyi Rais wa chemba ya Biashara Viwanda na kilimo(TCCIA) Wakati wa Mkutano wa siku moja wa Wafanyabiashara na wekezezaji zaidi 25 kutoka nchini Uturuki na wandani ya nchi ikiwa lengo Kubadilishana uzoefu na kupeana Fursa za Uwekezaji pande hizo mbili.

Koyi Amesema kuwa lengo la serikali nikuhakisha Wana wapa Fursa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Ndani ya nchi kutafuta masoko na kuwekeza nje ya nje ikiwa lengo kukuza Ushirikiano katika Uwekezaji.

Hata hivyo amesema kuwa Miongoni mwa mwa vitu wanavyo peleka nchini Uturuki ni Malighafi ya mazao hivyo basi wanaomba Wafanyabiashara kupeleka nchini humo kwa wingi na kuongeza ongezekao la thamani ikiwa lengo ni kuchochea Uchumi wa nchi na wakulima kwa Ujumla ili wanufaike na kilimo.

Wakati huo huo Amesema kuwa Miongoni mwa makampuni yalio kuja nchini kushiriki kutoka nchini Uturuki ni ya Umeme hivyo wamekutana na Wafanyabiashara Biashara wa Ndani wanaofanya Biashara ya vifaa vya Umeme hapa Tanzania ili wapeane Fursa za Uwekezaji.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafs TPSF Angelina Ngalula amesema kuwa Biashara ya nchi ya Uturuki na Serikali ya Tanzania imeendelea kukua na kufikia kipindi Cha Mwaka Mmoja Dola Milioni Mia Tatu tofauti na Zamani ilikuwa Dola Milioni Miambili na Hamsini Ndani ya Kipindi Cha Mwaka Mmoja imekua zaidi hivyo Kupitia juhudi Rais Jamhuli ya Muungano Wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani .

Aidha Bi. Ngalula amesema kuwa Uturuki Ina mpango wa kujenga Vituo vyao hapa Tanzania vya kuweza kuonesha Fursa ambazo zinapatoka nchini Uturuki kwa kushirikiana na Watanzania ili kuhakikisha wanachochoea Uchumi wa nchi hasa katika kuwainua Watanzania.

Mkutano huo ulifanyika Jijini Dar es salaam na Kushirikisha Wafanyabiashara na Wawekezaji Tofauti katoka Ndani nchi na nchi ya Uturuki ulio andaliwa na nchi ya Uturuki Chini ya Balozi wa nchi hiyo hapa nchini Mehmet Gulluoglu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live