Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa India walia muda mchache wa ‘Visa’

Wafanyabiashara India.jpeg Wafanyabiashara wa India walia muda mchache wa ‘Visa’

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

New Content Item (1) Mtwara. Baadhi ya wanunuzi na wasafirishaji wa korosho kutoka nchini India wameomba Serikali ya Tanzania kuwaongezea muda wa visa (kibali cha kuishi nchini) wanapokuja katika msimu wa korosho kutoka miezi mitatu wanayopewa sasa.

Akizungumza mbele ya Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan wakati wa ziara yake ya siku moja katika kikao cha wafanyabishara Narahari Prabhu amesema kuwa wanunuzi wengi wanapata visa ya miezi mitatu ambayo kwa sasa haitoshi.

“Unajua shida kubwa tunayo kwenye visa ambayo ni miezi miatu tunaomba serikali ituongezee muda wa kununua na kusafirish korosho miezi mitatu kwa sasa haitoshi ni michache” amesema Prabhu

Balozi wa India nchini Tanzania Binaya Srikanta Pradhan amesema kuwa amefika mkoani hapa ili kuweza kuangalia fursa za kibiashara zilipo.

“Unajua wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu nchini India walilifikisha suala la visa kwake na ameahidi kulifanyia kazi hivyo tuwe watulivu lakini kwa nchini kwetu huwa tunatoa viza za kibiashara kuanzia miezi sita na tunachaji fedha kidogo kama gharama za huduma” amesema Balozi Pradhan

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Revelian Ngaiza amesema kuwa kuongezewa kwa muda wa visa kwa wanunuzi ni sahihi kwakuwa muda wa uvunaji wa korosho umeongezeka kutoka miezi mitatu hadi tisa.

“Zamani Awali tulikuwa tunaanza msimu wa korosho tukiwa na miezi 3 ya uvunaji na sasa miezi 9 lakini sasa tumeongeza muda wa mavuno na pia mikoa inayolima korosho imeongezeka ndio maana wanaomba muda wa visa uongezwe” amesema Ngaiza

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa ujio wa balozi huyo ni fursa kwa nchi ambayo itawezesha wafanyabshara kuchangamkia fursa.

“Balozi amekuja kuona fursa mbalimbali ambapo ameona vifaa vikubwa vinavyoweza kusadia kupakia mizigo kwenye meli pamoja na eneo la kupakia meli” amesema Munkunda

Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara, Dunkan Kazibure amesema kuwa Bandari hiyo iko tayari kuhudumia shehena yote itakayohitaji kusafirishwa kupitia bandari hiyo.

“Sisi tuko tayari kuhudumia shehena yote itayofika hapa makasha yamefika na yataendelea kufika tumepanga ili tuweze kutoa huduma nzuri bandari yetu inauwekezaji mkubwa vifaa na watu wako tayari kufanyakazi” amesema Kazibure

Chanzo: www.tanzaniaweb.live