Wafanyabiasha waliounguliwa bidhaa zao katika soko la Ruaha Mikumi Wilaya ya Kilosa wameiomba Serikali kufanya mazungumzo na taasisi za fedha zilizowakopesha wafanyabiasha hao ili ziweze kuwaongezea muda wa kurejesha mikopo yao baada ya kupata hasara kufuatia moto uliounguza bidhaa zao.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiasha hao mwenyekiti wa wafanyabiasha, Ebu Lipenege amesema kuwa yeye ni miongoni mwa wafanyabiasha wenye madeni benki na walikuwa wakilipa madeni hayo kupitia biashara wanazofanya.
"Huu moto umetupa hasara kubwa maana mitaji yote imeteketea sasa bila ya msaada wa Serikali hizi benki na taasisi za fedha tulizokopa haziwezi kutuelewa, tunaomba Serikali itusaidie kututetea hata kama kutusamehe itashindikana basi tuongezewe muda wa kurejesha mikopo ama itupunguzie marejesho.
Aidha amesema kuwa mpaka sasa chanzo cha moto bado hakijafahamika na tathimini ya hasara inaendelea kufanyika.