Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara mitandaoni msitufanyie hivyo

49494 Julie+kulangwa

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara kadhaa nimejaribu kufanya manunuzi mtandaoni hasa Instagram kwa kuwa watangazaji wote wamehamia huko. Ni mara chache utakutana na tangazo la duka la mavazi, mgahawa au vipodozi katika mitandao mingine kama vile Facebook au Twitter.

Kwa kifupi maisha yamehamia Instagram. Ndani ya akaunti moja ya maarufu utakutana na matangazo ya bidhaa mbalimbali lakini sasa wengi ni feki.

Nilichogundua wengi wanaweka bidhaa ambazo hawana. Ukimfuata kwenye namba yake atakwambia hicho unachotaka kimeisha. Ni nafuu kwako kuamua kuulizia kabla ya kufunga safari kuifuata bidhaa hiyo katika duka lake.

Utakapoamua kwenda utakutana na vituko kwani wengi hawana vitu wanavyovionyesha kwenye akaunti zao. Kama ni duka la nguo utakutana na maronya ronya. Wengi hudownload picha kutoka katika mitandao lengo kupamba tu kurasa zao na siyo kweli wanazo.

Wapo wale wanaofanya udalali. Yaani muuzaji hana duka wala nini isipokuwa anapita kwenye maduka ya watu anapiga picha na kuziweka mtandaoni. Kimbembe ukimwambia sasa nataka kuja dukani nijaribishe kabisa hapo ndio utata unapokuja. Atarukaruka na ikibidi anakublock.

Kitu kingine nilichojifunza katika kufanya manunuzi ni kupata bidhaa ambayo haiendani kabisa na ulichokiona mtandaoni. Nikizungumzia hili mwanamuziki Shilole atakuwa ananielewa zaidi kwani mkasa alioupata kwa kuletewa gauni tofauti lilimfanya kituko cha mwaka.

Sidhani kama ni vyema mfanyabiashara kudanganya kuwa anayobidhaa fulani wakati hana.

Kuweka picha za bidhaa ambazo hana ni udanganyifu katika biashara kwa sababu watu huvutiwa na mwonekano. Inapotokea hivi mara mbili au tatu hukimbiza wateja.



Chanzo: mwananchi.co.tz