Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara kupewa maeneo ya bure soko jipya Temeke

Capturew Wafanyabiashara kupewa maeneo ya bure soko jipya Temeke

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kutekeleza kwa vitendo kauli ya Rais Samia ya kutaka Wamachinga wapangwe, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke chini ya Mstahiki Meya Abdallah Mtinika imetoa fursa ya Wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali kufanya biashara bure kwenye soko jipya la Kijichi (Kijichi Park) Wilayani Temeke.

Akizungumza wakati wa Tamasha la kuwakaribisha Wafanyabiashara lililofanyika kwenye Soko hilo, Meya Mtinika amesema wakati umefika sasa kwa Wafanyabiashara kuacha kufanya biashara Barabarani na wahamie kwenye Masoko ya kisasa yaliyojengwa kwa pesa nyingi na Serikali.

"Haina haja ya kupanga biashara kwenye mifereji njoo hapa tupo tayari kuwapatia maeneo mazuri, hii ni park kama ilivyo Mlimani City, tupo tayari kuwapa Wafanyabiashara miezi 6 ya kufanya biashara bure hapa, hata wale Wafanyabiashara wakubwa wa Supermarket n.k, anayetaka anaandika tu barua anamkabidhi Afisa Biashara wa Wilaya na tutaona namna gani tunamkabidhi eneo la biashara" Meya wa Temeke.

Nae Mbunge wa Jimbo hilo, Dorothy Kilave, amesema wameweka mkakati utakao wavutia watu kuja kwa wingi sokoni hapo, ikiw ani pamoja na kuweka sehemu ya michezo mbali mbali ambayo itakuwa ikifanyika kila mwisho wa juma.

"Tunatamani Wafanyabiashara wadogo waje, kila WeekEnd tutakuwa tunafanya michezo mbalimbali, tumeweka stand, burudani n.k, niwaombe Watu sio tu wa Temeke hata maeneo mengine waje hasa ambapo Mama (Rais Samia) anataka Wafanyabiashara wake sehemu salama" Dorothy Kilave, Mbunge wa Temeke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live