Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara kupewa dola Zanzibar

Dola Dola Juu Juu Wafanyabiashara kupewa dola Zanzibar

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Wafanyabiashara wa Zanzibar Ikulu Zanzibar na kusema Serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na upandaji wa bei za vyakula hasa mchele na sukari nchini.

Dk. Mwinyi amesema matarajio ya Serikali ni kurudisha bei za awali kwa bidhaa zilizopo MADUKANI ambapo ameagiza Serikali kutoa fedha zake za kigeni na kuwapa kipaumbele Wafanyabiashara hususan Waagizaji vyakula nje ya Nchi.

"Kwa hali tuliyofikia tusiposhirikiana huku mtaani hali inakua ngumu sana, bei zimepanda mno lazima tutafute njia juu chini, sisi tupo tayari kama Serikali kukusaidieni katika yale ambayo yapo ndani ya uwezo wetu fedha tulizokua nazo sisi kama Serikali dola zitolewe wapewe Waagizaji wa chakula,” amesema Rais Dr. Mwinyi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live