Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara kuanza kukopa nje ya nchi

TCCIAAA BIASHARAAA.png Wafanyabiashara kuanza kukopa nje ya nchi

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara nchi sasa wataanza kufanyiwa tathmini ili kuweza kupata mikopo kutoka nje ya nchi baada ya Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) kuingia mkataba na Wakala wa kimataifa wa kukadiria mikopo (ICRA).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Rais wa TCCIA, Vicent Minja amesema lengo kubwa ni kuwaunganisha wafanyabishara wa Tanzania na kuhakikisha sekta binafsi inapata nafasi yake na kupata mazingira mazuri ya kufanya kazi.

“Leo tunaidhinisha taasisi hii ambayo itatathimini makapuni na kusema kuwa huyu mtu anakopesheka au hakopesheki na kama anakopesheka ni kwa kiasi gani kwahiyo hawa ni wataalamu kwenye hayo mambo na wamesajiliwa na benki kuu na wanafanya hivi na nchi zingine ni kampuni kubwa inayotambulika,” amesisitiza.

Ameeleza kuwa TCCIA imeingia makubaliano hayo na wanachama ili waweze kukidhi vigezo ambavyo wanaweza kukopeshwa ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live