Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara binafsi wa mafuta wapewa ushauri na EWURA

Wafanyabiashara Binafsi Wa Mafuta Wapewa Ushauri Na EWURA Wafanyabiashara binafsi wa mafuta wapewa ushauri na EWURA

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara binafsi wanaouza mafuta wametakiwa kuingia mikataba na wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mafuta nje ili wawe na uhakika wa upatikanaji wa mafuta na kuondoka shida ya kukosekana mafuta katika vituo vyao.

Aidha endapo wafanyabiashara hao wataingia mikataba hiyo itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la upatikanaji wa mafuta kwa wafanyabiashara binafsi wanaouza mafuta jambo ambalo linawapelekea mafuta kukosekana katika vituo vyao na wananchi kuteseka.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha na Meneja wa EWURA kanda ya kaskazini ,Lorivii Long’idu wakati akiongea na wafanyabiashara binafsi wa mafuta katika kikao kazi kilichoandaliwa na EWURA kikiwa na lengo la kukumbushana taratibu za ufanyaji biashara ya uuzaji wa mafuta kikao kilichowashirikisha wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Amesema kuwa, kikao hicho kimeandaliwa kwa ajili ya kuweza kuwakumbusha wafanyabiashara hao wajibu wao wa kuwauzia wananchi mafuta bila kubagua na kufuata taratibu na sheria maana kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa hawafuati taratibu na sheria za ufanyaji wa biashara ya mafuta.

“Nawataka wafanyabiashara hawa kuwa na mikataba na waagizaji mafuta lengo la mikataba ni kuwawezesha kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta, sababu hawa waagizaji mafuta wakubwa wana tabia moja, unapoagiza mafuta lazima wajue hayo mafuta wanamuuzia nani na kuna ambao wana mikataba na sisi tunayo ili tuweze kufuatilia lakini pia kuna ambao hawana mikataba na wengi wao ndio wanakosa mafuta na kuanza kulalamika,” amesema Lorivii.

Amesema, lengo la mikataba hii ni kuhakikisha kwamba bidhaa ya mafuta inapoagizwa, hawa wafanyabiashara wakubwa kujua wanakwenda kuwauzia wafanyabiashara binafsi kwa utaratibu gani, ili huduma ya mafuta iweze kuwafikia wananchi kwa wakati na maeneo ya mbali zaidi.

Nao baadhi ya wafanyabiashara binafsi waliohudhuria kikao hicho wamesema kuwa kuna baadhi yao wana mikataba na wafanyabiashara hao wakubwa lakini wamekuwa wakikosa huduma ya mafuta huku wengine wakizungushwa kupata mafuta hayo na wengine wakiambiwa walipe fedha mara mbili.

“Unakuta mimi nimelipia mafuta leo kwa huyo mfanyabiashara mkubwa na nina mkataba lakini cha kushangaza nikitaka mafuta nazungushwa muda mwingine naambiwa niongezee fedha mafuta yamepanda la sivyo nirudishiwefedha au unakuta kuna mtu anataka nitoe cha juu ili nipate ukiangalia kituo changu cha mafuta hakina mafuta ,na unakuta wateja wetu wakubwa wanakuja lakini wanakosa mafuta imekuwa ni changamoto kubwa sana," amesema Mfanyabishara wa mafuta kutoka mkoani Tanga Marco Masanja.

Aidha, wafanyabiashara hao kwa pamoja wameomba serikali kukaa na wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mafuta kupanga bei ambayo itakuwa haimnyimi faida muagizaji na ambayo haita muumiza mwananchi kwani kwa sasa hivi bei iliyopangwa inamuumiza muagizaji na ndio maana baadhi yao hawauzi mafuta kwa wafanyabiashara ambao ni binafsi kwa kukwepa hasara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live